Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twiga Stars waanza vyema Kombe la COSAFA

Twiga Stars COSAFA.jpeg Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Tanzania wameanza vyema michuano ya COSAFA kwa wanawake baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Comoro mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Madibaz mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini.

Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na Donisia Minja dakika ya 13 na Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ mawili dakika ya 41 na 52.

Baada ya mechi hiyo, nyota wa Twiga Stars Enekia Kasonga ‘Lunyamila’ alipewa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa soka nzuri aliyoonyesha huku akitoa mchango mkubwa kwa ushindi wa timu yake kutokana na kufunga mara mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live