Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twiga Stars ni kushambulia tu Botswana

Twiga Stars Kikosi Vs Botswana Twiga Stars ni kushambulia tu Botswana

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Katika kile kinachoonekana hana hofu na mchezo wa ugenini leo dhidi ya Botswana wa marudiano ya kuwania kufuzu michezo ya Olimpiki mwakani, kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars', Bakari Shime ameanzisha kikosi chenye washambuliaji wanne.

Tofauti na mchezo wa kwanza nyumbani ambao Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambapo kocha Shime alianzisha washambuliaji watatu kikosini, leo amewaanzisha kwa pamoja Stumai Abdallah, Winfrida Gerard, Oppa Clement na Aisha Masaka.

Uwezo wa Aisha Masaka anayechezea BK Hacken ya Sweden kusimama katika nafasi ya mshambuliaji wa kati, unaashiria kwamba Oppa anayecheza soka la kulipwa Uturuki katika timu ya Besiktas, Winfrida Gerard na Stumai ambao wanaichezea JKT Queens watakuwa wakicheza mechi ya leo kwa kubadilishana katika nafasi za mshambuliaji namba 10, winga wa kulia na winga wa kushoto.

Kocha Shime kama ilivyokuwa katika mechi iliyopita, ameendelea kumpa nafasi ya kipa namba moja, Najiat Abbas ambaye safu yake ya ulinzi inaundwa na mabeki Happyness Mwaipaja, Julietha Singano, Annastazia Katunzi na Diana Mnally.

Safu ya kiungo ya Twiga Stars itawategemea Joyce Lema na Diana Lucas ambao nao wameanzishwa na kocha Shime.

Katika mchezo wa leo, Twiga Stars inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele.

Chanzo: Mwanaspoti