Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twiga Stars kukamilisha makundi na Sudani Kusini

4407ed0dddb4cfd7e8a90565c7bf0d9e Twiga Stars kukamilisha makundi na Sudani Kusini

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' leo itakamilisha mechi za hatua ya makundi za michuano ya Cosafa inayoendelea nchini Afrika Kusini kwa kucheza na Sudani Kusini.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari Shime, amesema maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kuanza majira ya saa 7: 00 kwa saa za Tanzania yamekamilika na matumaini yao ni kushinda mchezo huo.

"Maandalizi yetu kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa asilimia zote wachezaji wangu wote wapo katika hali nzuri na lengo letu ni kushinda ili kumaliza vinara kwenye kundi B, " amesema Shime

Twiga Stars inayoshiriki michuano hiyo kama timu mwalikwa mpaka sasa imecheza mechi mbili dhidi ya Zimbabwe na Botswana na kushinda zote na kocha Shime amesema lengo lao ni kurudi na Kombe hilo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz