Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania ‘Twiga Stars‘ inatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Sudan Kusini na Mali, mwishoni mwa mwezi huu ikiwa sehemu ya maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika, nchini Morocco.
Michezo hiyo inatarajiwa kuchezwa Mei 29 hadi 30, mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Dar es Salaam. Twiga Stars kinaendelea kufanya mazoezi yao katika kituo cha ufundi cha Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kilichopo, Kigamboni.
Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema leo wanapokea timu tatu za wanawake kutoka Sudan Kusini, Mali na Sychelles kwa ajili ya mechi za kirafiki.
“Kila timu itapata nafasi ya kucheza mechi mbili ambazo ni kwa ajili ya kujiandaa na mashindano yaliyopo mbele yao, mataifa haya ni makubwa sana na inaonyesha jinsi gani soka la wanawake linavyozidi kukuwa.
Kuhusu timu ngeni tayari zimewasili na waamuzi watakaochezesha mechi hizo watakuwa watanzania, hii ni kuendeleza soka la wanawake limazidi kukuwa,” amesema Ndimbo.
Kuhusu wachezaji wanaocheza soka la kulipwa, Ndimbo amesema nyota wote wamewasili na wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya michezo hiyo miwili ya kirafiki.
Kikosi cha Twiga Stars ni Najat Abbas, Lidy Maximilian, Christer Bahera, Janeth Panhamwene, Vaileth Nicholas, Maimuna Kaimu, Joyce Lema. Jamila Rajabu, Winifrida Gerald na Stumai Abdallah (JKT Queens), Asha Mwisho. (Amani Queens), Enekia Kasongo (Easter Flames. Saudi Arabia).
Wengine ni Julitha Singano (Juares, Mexico), Suzan Adam (Tuthankhamu, Misri), Diana Lucas (Ame D.F.K, Uturuki), Oppa Climate (Besikta, Uturuki), Aisha Masaka (BK Häcken. Sweden) na Clara Luvanga (Al Nasir FC. Saudi Arabia), Aisha Mnuka (Simba) na Asha Ramadhan (Yanga Princess).
Twiga Stars ambayo Februari mwaka huu hawakufanya vizuri na kuondolewa kwenye michuano ya kufuzu Olimpiki dhidi ya Afrika Kusini .
Twiga Stars ilitupwa nje ya michuano hiyo kwa jumla ya mabao 4-0, walikuwa kichapo cha 3-0 nyumbani kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi Dar-es-Salaam na 1-0 katika mchezo wa marudiano nchini Afrika.