Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twiga Stars balaa, yaichapa goli 2 Botswana

Twiga Wanawake Taifa Kikosi cha Twiga Stars Kikishangilia goli dhidi ya Botswana

Sat, 2 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa Magoli 2-0 dhudi ya Botswana katika mashindano ya COSAFA WOMEN 2021, yanayoendelea nchini Afrika ya Kusini.

Twiga Stars inashiriki kama mwalikwa katika mashindano hayo na mara kwa mara wamekuwa wakiibuka na ubingwa katika michuano hiyo ya COSAFA.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mndela Bay, Mjini Port Elizabeth ulishuhudia Twiga wakionyesha kiwango cha kuvutia na kuibuka na ushindi huo.

Magoli ya Twiga Stars katika mchezo huo, yamefungwa na Donisia Minja dakika 6' na Mwanahamis Omary 79'.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, kocha wa Twiga Stars Bakari Shime amesema;

"Mchezo ulikuwa mgumu kutokana na hali ya uwanja, upepo mvua kwa hiyo ilituchukua muda mrefu kuweza kupata uelekeo wa mchezo"

"Nilichowaambia wachezaji wangu ni kutulia, wacheze vile tunavyotakiwa kucheza na mwisho wa mchezo tumefanikiwa kuwa washindi" amesisitiza Shime.

Mchezaji wa Twiga Stars , Fatma Issa, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika mtanange hu.

"Nafurahi kupata tuzo hii ya mchezaji bora kwani sio ya kwangu ni ya Watanzania wote kwa kuwa wanatupa sapoti, na wachezaji wenzangu pia tunapambana uwanjani ila kwa kuwa hii tuzo iko moja tu leo ni kwangu na kesho itakwenda kwa mwingine

Chanzo: www.tanzaniaweb.live