Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twaha Kiduku kuzitwanga na Sebyala

Twaha Kiduku Morogoro Twaha Kiduku kuzitwanga na Sebyala

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Twaha Kiduku kutoka Tanzania anatarajia kuvaana na bondia kutoka Uganda Mohammed Sebyala Desemba 26, 2023 kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam na ikitarajiwa kuwa mabondia 20 wa ngumi za kulipwa watapanda ulingoni siku hiyo ambapo, Desemba Mosi baadhi yao akiwamo Kiduku wamesaini mkataba na muandaaji wa mapambano hayo, kampuni ya Peaktime Sports Agency.

Hayo yamesemwa jijini Dar Es Salaam na mratibu wa matukio kutoka kampuni hiyo Bakari Khatibuna kusema kuwa siku hiyo watakuwa wanaadhimisha miaka mitano ya Usiku wa Mabingwa, pia ni sherehe ya kutambua mchango wa mabondia waliofanya vizuri.

“Hii ni sherehe ya kutambua mchango wa mabondia ambao tumefanya nao kazi na waliofanya kazi na mapromota wengine lakini kwa mwaka 2023 wamefanya mema katika mchezo wa ngumi,” ameeleza Khatibu.

Naye bondia Kiduku ameishukuru Peaktime kumuandalia pambano hilo baada ya kupoteza mechi yake ya mwisho aliyopigana na bondia kutoka Afrika Kusini na kusema kipindi hiki hatafanya makosa lazima ushindi ubaki nyumbani.

“Namshukuru Meja Semunyu kwa kunipa pambano hili, nimelipokea kwa hamu. Niwaambie tu yule Msauzi atawaponza wengi, amemkanyaga nyoka mkia,” amesema Kiduku.

Bondia Mkongwe Fransic Miyeyuso ambaye anapigana na Saidi Bwanga, ametamba kuwa yeye bado yuko vizuri ndiyo sababu mabondia wachanga wanamkimbilia hivyo ataonyesha mchezo mzuri.

Kwa upande wake bondia wa kike Jesca Mfinanga anayecheza dhidi ya Sara Alex, amesema kupewa nafasi ya kucheza siku hiyo ina maanisha ameonekana yeye ni bingwa na atamuonyesha kazi mpinzani wake.

Mabondia wengine watakaozichapa siku hiyo Oscar Richard dhidi ya Sabelo Ngebinyana kutoka Afrika Kusini, Maono Ally na Joseph Maigwisa, Hassan Ndonga atatwangana na Gabriel Ochieng wa Kenya, Ally Ngwando.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live