Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuzo za TFF zitolewe mapema kuzipa thamani

Tuzo Wafungaji Tuzo za TFF zitolewe mapema kuzipa thamani

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wa tuzo za msimu za (TFF) Ligi Kuu Tanzania Bara zinafanyika msimu wa 2021-2022 na 2022-2023 wachezaji wengi walikuwa tayari wameondoka kwenye timu zao kwenda likizo.

Wachezaji wengi hasa wa Kimataifa walilazimika kuwatumia wachezaji wenzao kuwawakilisha kwa ajili ya kupokea tuzo hizo lakini utakubaliana na mimi kwamba ni heshima kubwa iwapo mhusika akapokea tuzo yake yeye mwenyewe japo si mbaya kuwa na mwakilishi.

Ili kuzipa tuzo heshima zinazostahili, kwa nini msimu huu tuzo zisitolewe mapema kabla ligi haijatia nanga ili wachezaji husika kwenye tuzo wahudhulie wote kuliko kusubiri hadi mechi ya fainali ya (FA) Juni 2, 2024 ipite hali itakayofanya kuwakosa baadhi ya nominies ambao watakuwa wameshaenda likizo baada ya ligi kuu kufika ukingoni Mei 28.

Ushauri wangu ni kwamba, kuiga kitu kizuri sio dhambi, wenzetu walioendelea tuzo zao za ligi kuu hutolewa kabla au siku ya mwisho ya mechi za ligi kuu.

Kama mkikaza fuvu hiyo tarehe mliyopanga hamtawapata hao nominees, wachezaji watakuwa wameenda likizo na wengine kwenye timu za taifa,As usual tuzo watapokea viongozi wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live