Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuzo za Ballon D'Or ni biashara tu - Kiemba

Tuzo Za Ballon D'Or Ni Biashara Tu   Kiemba Tuzo za Ballon D'Or ni biashara tu - Kiemba

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Kiemba amezungumzia tuzo ya Ballon D'Or aliyoshinda Muagentina, Lionel Messi.

Kiemba anasema kwa mtazamo wake anaona waandaji wamekuwa wakizitumia kibishara kulingana na wao wenyewe wanavyoona.

“Hizi tuzo ni utashi wa walioandaa tuzo wenyewe, nakumbuka hata msimu ulioisha ilikuwa hivi hivi alionekana Lewandowski anastahili akaandaliwa tuzo nyingine, naona ni biashara tu.

“Walioandaa wakiona wanayetaka ashinde hana vigezo hivi wanabadilisha vigezo," alisema Kiemba.

Mshambuliaji huyo wa Argentina na Inter Miami ameshinda Tuzo ya Ballon d'Or kwa Wanaume kwa mara ya nane.

Messi mwenye umri wa miaka 36 alitambuliwa katika sherehe hiyo mjini Paris baada ya kuisaidia nchi yake kushinda Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live