Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuzo yampa mzuka Junior

Waziri Junior Kmc Tuzo yampa mzuka Junior

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba, msimu huu, mshambuliaji Waziri Junior wa KMC amesema imezidi kumtia hasira ya kufanya vizuri katika mashindano yote ambayo timu yake inashiriki.

Junior ameshinda tuzo hiyo akimzidi mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke na John Nakibinge wa Tabora United.

Junior amesema kitendo cha kushinda tuzo hiyo kwake ni mara ya tatu hivyo inampa nguvu ya kupambana kuisaidia timu yake kufanya vizuri katika msimu huu.

Mshambuliaji huyo amesema kila mchezaji anapenda kufunga, hivyo kama ataendelea kupata nafasi ya kucheza atatimiza wajibu wake ipasavyo.

"Tuzo hii imezidi kuniamsha kama mchezaji kuendelea kufanya vizuri katika timu yangu. Nitatumia kila nafasi ninayoipata kuweza kufanya vizuri," amesema Junior.

Mshambuliaji huyo amefunga mabao mawili katika mechi mbili mfululizo dhidi ya JKT Tanzania na Geita Gold.

Katika msimu wa 2019/20 akiwa na Mbao FC ya Mwanza, Junior alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Julai wakati timu hiyo ilipocheza michezo mitano na kupata sare moja, huku mshambuliaji huyo akifunga mabao matano na kutoa pasi moja ya bao akiwashinda Peter Mapunda aliyekuwa Mbeya City na Obrey Chirwa aliyekuwa Azam FC.

Msimu huohuo alichukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Novemba akifunga mabao manne katika mechi sita ambazo alicheza na alimaliza akiwa amefunga mabao 12 na kuwafanya mabosi wa Yanga kuinasa saini yake.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: