Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tutegemee sura mpya, Simba ikiwavaa Namungo

Simba Sporyts Tr Simba SC, Mazoezini Bunju ,Dar

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu kunako Kikosi cha wekundu wa Msimbazi, Thierry Hitimana amedikeza kuwa anatarajia kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao hawakucheza kwenye michezo iliyopita ya Ligi Kuu Bara.

“Siwezi kubadilisha ghafla kikosi kilichokuwa kinaanza kwani bado nahitaji muda wa kukiandaa kikosi changu kwenye michezo ijayo, huku nikijaribu kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji wengine.

“Mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union hatukuwa na mchezo mzuri, ila nikaanza na Jonas Mkude kwa kumpatia nafasi kipindi cha pili na aliweza kufanya kazi nzuri katika eneo la kiungo

“Hivyo katika michezo ijayo tutarajie kuwaona baadhi ya wachezaji uwanjani kama vile Patrick Mwenda, Kennedy Juma pamoja Jimson Mwanuke,” alisema Hitimana ambaye za ndani kabisa zinasema amewaambia viongozi walete Kocha Mkuu tu yeye ataendelea kuwa msaidizi.

Simba imecheza michezo miwili chini ya Hitimana ikishinda mmoja kwa kuifunga Polisi Tanzania na kutoka suluhu na Coastal Union. Mechi zote zimecheza katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Hitimana alikuwa kocha msaidizi chini ya Didier Gomes aliyetimuliwa wiki iliyopita na sasa anasaidiana na Seleman Matola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live