Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tutamfanya vibaya Wydad - Simba

Ahmed Ally Semaji La Simba.jpeg Tutamfanya vibaya Wydad - Simba

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC, wamesema watahakikisha wanamfunga kwa idadi kubwa ya magoli Wydad katika mechi yao ya nne ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika Desemba 19, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Kauli hiyo ya kishujaa imetolewa na Semaji la CAF, Ahmed Ally alipokuwa kwenye uwanja wa Azam Complex-Chamazi jijini Dar mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Simba Queens na JKT Tanzania.

Kwenye mechi hiyo ambayo ilikuwa ya Ngao ya Jamii, Simba Queens aliibuka kidedea kwa mikwaju ya penalti 5-4.

"Wydad inabidi achakae vibaya mnoo, achakae kwa namna ambayo hajawahi kuchakaa.... Safari hii akija Benjamin Mkapa sio afungwe kagoli kamoja afungwe kwa namna ambayo hajawahi kufungwa, tutamfanya vibaya Wydad, kikubwa wanasimba mjiandae kwenda uwanjani," alisema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live