Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tutalipa kisasi kwa Zambia- U-17

51d8a2ad4372ae9cdc430b221698dfbf.jpeg Tutalipa kisasi kwa Zambia- U-17

Sat, 14 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

FAINALI ya michuano ya Cosafa inatarajiwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa Wolfson, Port Elizabeth, Afrika Kusini huku wachezaji wa timu ya wanawake ya Taifa ya soka ya umri chini ya miaka 17 wakiapa kurudi na kombe kama walivyofanya timu ya U20 mwaka jana.

U17 inayofundishwa na kocha Edna Lema imefuzu fainali baada ya kuifunga Comoro 5-1, Afrika Kusini 6-1 na Zimbabwe 10-1 na kufungwa mchezo mmoja na Zambia kwa 2-1 ambao ndio watakaocheza nao fainali.

Akizungumza jana nahodha wa timu hiyo Irene Kisisa alisema wamejiandaa vizuri na waamini watarudi na kombe kama walivyofanya timu ya U20 ilipoalikwa mwaka jana.

"Mwaka jana dada zetu wa U20 walirudi na kombe baada ya kuifunga Zambia na sisi tunacheza tena fainali na Zambia, tuna imani tutawafunga tulipe kisasi na kuchukua ubingwa, " alisema Irene.

Alisema Zambia hawawezi kuwafunga mara mbili lazima walipe kisasi kwani makosa yaliyosababisha wakafungwa kocha aliyafanyia kazi na pia wanazitaka dola 15,000 walizoahidiwa na kamati ya ushindi ya Taifa Stars.

Naye kocha Edna alisema wachezaji wana morali na wamefanya mazoezi tangu juzi na hakuna majeruhi hivyo watanzania wawaombee ili wafanikishe azma ya kurudi na kombe.

"Tunaimani tutaifunga Zambia na wachezaji wana ari kwani wanataka kulipa kisasi, kikubwa watanzania watuombee," alisema Edna.

Mashindano ya Cosafa yanahusisha timu 10 za wakubwa za wanawake na tano za wasichana U17 yanatarajiwa kumalizika leo

Kwa upande wa timu za wakubwa fainali itakuwa kati ya Afrika Kusini na Botswana, Afrika Kusini ilifuzu baada ya kuifunga Malawi na Botswana ikiifunga Zambia.

Baada ya mchezo wa fainali U17 itaanza safari ya kutoka Port Elizabeth saa 10:00 kwa basi kwenda Johanesburg tayari kurejea nyumbani na inatarajia kufika Tanzania, usiku wa kesho.

Chanzo: habarileo.co.tz