Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tutakula pilau la Krismasi Chamazi-Yanga SC

Ally Kamwe Kijembe Tutakula pilau la Krismasi Chamazi-Yanga SC

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tayari joto la Mzizima Dabi limeshaanza kupanda! Yanga SC wamewatambia wapinzani wao Azam FC kwa kuwaambia kuwa watakula pilau katika Uwanja wao siku hiyo.

Yanga wanatarajia kukutana na Azam siku ya Krismasi Desemba 25, 2022 katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar kama hakutakuwa na mabadiliko ya Uwanja.

Afisa Habari ya Yanga, Ally Kamwe amesema, Wana mechi mbili kabla ya kukutana na Azam lakini wanafahamu kwamba siku hiyo ya Krismasi itakuwa ni siku ya kuwatembezea kichapo Azam.

"Tuna mechi na Polisi Tanzania lakini pia tuna mechi na Coastal Union na Kisha itakapofika siku ya sikukuu ya Krismasi, tuna jambo letu na Azam FC.

Mayele atakuwa na kazi maalum ya kulambisha ice cream na siku hiyo sisi pilau tutalibeba kwenye ma-hotpot tutakwenda kulia palepale Chamazi kama hawajabadilisha uwanja maana huwa wanabadilisha. Sisi popote tunawasikiliza wao," alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live