Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Tutaipiga Simba kwenye mshono"- Polisi Tanzania

POLISI TANZANIA Kikosi cha vinara wa Ligi, Polisi Tanzania

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Polisi Tanzania hii leo Oktoba 27, majira ya saa 1:00 usiku watashuka katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam kukabiliana na bingwa mtetezi Simba SC katika Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Primia Ligi).

Polisi Tanzania inaingia katika mchezo huo ikiwa na rekodi nzuri ya kushinda kwa 100% michezo yake msimu huu kwani imecheza michezo mitatu na kushinda yote.

Katika msimamo wa Ligi, Polisi Tanzania ndio vinara wakiwa na alama tisa mpaka sasa.

Wakati wanaenda katika mchezo huo jioni ya leo wameitahadharisha Simba kuwa wasitarajie ushindi katika mchezo wa leo, Simba ambayo imetoka kupoteza katika uwanja huo huo kwa magoli 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Simba itakua chini ya kocha mpya katika mechi hiyo Hitimana Thiery , baada ya kuachana na Didier Gomes Da Rosa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live