Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Tutafanya kwa Mkapa kuwa machinjioni"- Poulsen

Kim Poulsen Kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni mipango juu ya mipango kwa Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen katika kuisuka Stars kufuzu kwa Fainali za kombe la Dunia Qatar 2022.

Stars juzi iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar, mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022, zitakazofanyika nchini Qatar.

Akizungumza baada ya ushindi huo, Poulsen alisema anaamini kila mechi ni muhimu kupata matokeo mazuri na malengo yake ni kuona anatumia vema uwanja wa nyumbani kuwa sehemu ya machinjioni kwa timu ngeni zitakazokuja kucheza, dhidi ya Stars.

"Niwapongeze sana wachezaji kwa kufuata maelekezo yangu baada ya kwenda mapumziko tukiwa 2-2, wakati tulipokuwa tunaongoza, walirudi nyuma jambo ambalo halitakiwi katika soka, niliwaeleza tunaenda kipindi cha pili kuhakikisha tunashambulia na kushambulia, jambo ambalo tumefanikiwa kupata ushimdi.

"Jambo lingine nimewasisitizia kwa sasa tunataka kutumia Uwanja wa Benjamini Mkapa kuwa sehemu ya machinjio kwa yeyote anayekuja, hatoki na ushindi," amesema Poulsen.

Amesema ameona mabadiliko makubwa kwa wachezaji wake kuongeza kujiamini na kufuata maelekezo anayowapa, hivyo kuwataka kutumia vema uwanja wa nyumbani kupata matokeo mazuri katika mechi watakazocheza kwa Mkapa.

"Kwa kujiamini kwa wachezaji wangu, natarajia mechi zijazo kucheza vizuri na kutafuta matokeo, kwa sababu wapinzani tunakutana nao (Benin) ni wagumu," amesema kocha huyo.

Matokeo hayo yanaifanya Stars kukaa kileleni mwa Kundi J ikiwa na pointi nne sawa na Benin, ambayo wanalingana hadi tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live