Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Tutadili na kila mchambuzi, kila andiko"- Manara

Manara FULL MAJIGAMO Viongozi wakuu Kitengo cha Habari na Mawasilano Yanga

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa mnayo? Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema kuwa hivi sasa waandishi na wachambuzi wote wanaoiandika na kuisema vibaya Yanga wajiandae kwa kuwa mkakati uliopo ni kushughulika nao.

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari, kuelekea mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting, amesema wanaanda vijana ambao atawafundisha yeye mwenyewe, na kazi yao kubwa itakua ni "ku-deal" na waandishi na wachambuzi wote wanaoisema au kuiandika vibaya Yanga.

"Sasa hivi labda tu niwaambie, tutashughulika na kila andiko, kila kauli itakayoizungumza Yanga hovyo, muda wa kuwaogopa ogopa na kuwalea lea umekwisha sasa hivi tutashughulika nao"

"Tutaandaa vijana na mimi ndio ntakaowafundisha kwa sababu naziweza hizi kazi nishakaa kwenye media muda sana, wao watakua na jukumu hilo la kumalizana na hao mnaowaita wachambuzi" amesisistiza Manara

Yanga inashuka dimbani kwa Mkapa jioni ya leo, Novemba 2 kupepetana na Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live