Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tusubirie kuona Wasenegal wataisadia vipi Azam FC

Azam FC Makocha Wawili Tusubirie kuona Wasenegal wataisadia vipi Azam FC

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wanetu Azam FC hawataki mchezo na sasa ameamua kivingine kwa kuajiri benchi la ufundi kutoka Senegal ili kuinoa timu hiyo katika msimu ujao.

Kocha mkuu anatoka Senegal pamoja na wasaidizi wake wakiwemo kocha wa makipa pamoja na mtaalamu wa kufanya tathmini ya viwango vya wachezaji katika mechi na mazoezini.

Naam ndio mahitaji ya soka la kisasa hayo yanataka hivyo kwamba kocha anakuja na wasaidizi wake ili kuifanya timu iimbe lugha moja na hata panapokuwa na uwajibishwaji basi wote kwa pamoja wanalazimika kuwajibika.

Hii ina faida zake, kama hiyo niliyoitaja hapo juu lakini pia ina faida kuendelea na maisha yaleyaley pindi kocha mkuu anapokosekana kwani wasaidizi wake watafanyia kazi vyema mpango kazi wake ambao anaandaa kwa mechi husika.

Lakini hasara za kuchukua watu wengi kutoka taifa moja ni kuleta ubaguzi ndani ya timu na mpasuko pindi mambo yanapokuwa hayaendi sawa. Ni rahisi kushawishiana pindi kunapotokea mgomo na hata kuhujumu timu.

Bila shaka Azam FC imezingatia tathmini ya faida na hasara inayoweza kuzipata kwa kuajiri benchi la ufundi kutoka nchi moja hivyo imejiridhisha kuwa inapaswa kufanya hivyo.

Kwa sisi watu wa mpira tuliopo nje ya timu, hatua namna zaidi ya kukaa pembeni na kuona nini ambacho Azam FC itakipata ikiwa chini ya raia hao wa Senegal ambao imewapa jukumu la kuinoa timu hiyo.

Waliwahi kujaribu kuchukua benchi la ufundi kutoka England, wakafanya hivyo kwa makocha kutoka Hispania, Burundi na na baadaye ikawachukua kutoka Marekani lakini hatukona mabadiliko makubwa. Labda upepo unaweza kuwa mzuri kwa hawa Wasenegal.

Chanzo: Mwanaspoti