Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tusker wakutana na kichapo cha kwanza Ligi Kuu

Bandari Celebration Tusker wakutana na kichapo cha kwanza Ligi Kuu

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vinara wa Ligi Kuu nchini Kenya KPL Tusker FC wamekutana na kichapo cha kwanza kwenye Ligi msimu huu cha bao 2-1 mbele ya Bandari FC katika mchezo wa Ligi uliochezwa uwanja wa Bandari, Mbaraki Sports Club.

Tusker ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi la Kenya walikuwa hawajapoteza kwenye mechi takribani nane ambazo wamecheza msimu huu kabla ya kujikwaa kwenye kigingi cha watukutu Bandari.

Ushindi wa Bandari unawafanya wakamate nafasi ya 10 kwenye msimamo wa KPL baada ya michezo saba wakati Tusker wakiendelea kushika nafasi ya kwanza alama 18 mechi saba pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live