Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tusipochangia kadi ya uanachama tusilaumiane Aziz Ki akiondoka - Kamwe

Kamwe Na Aziz Tusipochangia kadi ya uanachama tusilaumiane Aziz Ki akiondoka - Kamwe

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe amewaambia mashabiki wa Yanga wanaouliza kuhusu hatma ya kiungo wao mshambuliaji Aziz Ki, badala ya kumanya hivyo, walipie ada zao za uachama.

Kamwe ameyasema hayo leo Mei 22, 2024 alipokuwa akielezea shamrashamra za ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC utakaonza kusherehekewa Ijumaa hii Mei 25, 2024 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Tusidanganyane ndugu zangu hawa wachezaji ni kweli wanatakiwa na timu kubwa tena sio hapa Tanzania maana hakuna timu yenye hela zaidi yetu sasa basi sisi tulipie ada zetu ili tuweze kuwabakisha wachezaji hawa wakubwa kwenye timu yetu," alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live