Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tusimfananishe Gamondi na Nabi - Jembe

Nabi Gamondi 2 WA0002 Tusimfananishe Gamondi na Nabi - Jembe

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Legend kwenye masuala ya habari za michezo Bongo kitaifa na kimataifa, Saleh Ally Jembe amefungukia kuhusu uwezo wa Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi dhidi ya aliyekuwa Kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi.

Jembe amesema Gamondi ambaye amecheza mechi sita mpaka sasa akiwa na Simba na kuonyesha uwezo mubwa bado hawezi kufananishwa na Nabi ambaye alichukua makombe yote ya ndani kwa miaka miwili mfululizo hivyo watu wanapaswa kumpa nafasi Gamondi ili afanya makubwa.

“Ligi haiwezi kumalizwa na mechi moja, Yanga wamecheza mechi moja tu ya Ligi dhidi ya KMC hawajacheza na timu nyingine hata KMC wamecheza na Yanga pekee hawajacheza na timu nyingine kwa hiyo huwezi kusema watafungwa mechi zote kama walivyofungwa na Yanga.

“kumlinganisha Gamondi na Nabi bado ni mapema sana, gamondi alikuwa anacheza mpira mzuri na kuchukua makombe lakini Gamondi anacheza mpira mzuri pia licha ya kwamba hajachukua kombe hata moja na tayari amepoteza kombe moja la Ngao ya jamii ambalo alilileta Nabi.

“Nabi amewahi pia kushinda bao tano kama alivyofanya Gamondi, nadhani mwisho wa msimu tunagalie makombe kwanza badala ya kufuata matokeo ya mchezo mmoja tu. Sio timu zote atakazokutana nazo yanga zitakuwa na makossa kama waliyofanya KMC.

“Yanga wametengeneza nafasi na kuzitumia vizuri kwa zaidi ya asilimia 90 tofauti na mechi ya Simba, kwa hiyo gamondi kuna kitu amekibadilisha kuanzia mechi ya kwanza.

“Nabi ni Nabi na Gamondi ni Gamondi, huyu anatoka Tunisia mwingine Argentina ni watu wawili tofauti, Gamondi anataka timu yake ishambulie zaidi tofauti na Yanga ya Nabi.

"Yanga hawajaruhusu bao maana yake ni wazuri kwenye kujilinda tofauti na Simba ambao tayari wamesharuhusu mabao. Yanga ndiyo timu ambayo imeanza vizuri Ligi Kuu msimu huu, naamini muda utaongea," amesema Jembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: