Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tusila Kisinda arejea Yanga

KISINDA Dfff Tusila Kisinda arejea Yanga

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Young Africans SC imetangaza kukamilisha usajili wa winga wa kushoto, Tuisila Kisinda mwenye umri wa miaka 22 kutoka Renaissance de Berkane ya Morocco.

Kupitia mtandao wa Kijamii wa Instagram, Mwenyekiti wa Yanga, Hersi Said ameonekana akifanya maongezi mafupi na Kisinda kuashiria kuwa mchezaji huyo raia wa DR Congo amerejea nyumbani kwa mara nyingine.

Young Africans imetangaza ingizo jipya hilo muda mfupi kabla ya Dirisha Kubwa la Usajili la Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu wa 2022/2023 kufungwa rasmi August 31,2022.

Kisinda anarejea Yanga SC akitokea RS Berkane ya Morocco iliyomsajili kutoka Yanga August 13, 2021 pamoja na Clatous Chama wa Simba SC.

Usajili huo unaifanya Yanga SC kuwa na Wachezaji zaidi ya 12 wa kigeni ambao ni;

1:Fiston Mayele

2:Yanick Bangala

3:Djuma Shabani

4:Jesus Moloko

5:Djgui Diarra

6:Khalid Aucho

7:Lazaraus Kambole

8:Stephen Azizi Ki

9:Joyce Lomalisa

10:Gael Bigirimana

11:Bernard Morrison

12:Heritier Makambo na

13:Tuisila Kisinda

Jesus Moloko anatajwa kutolewa kwa mkopo ili wabaki 12 ambapo wanaruhusiwa kutumiwa kwenye Michezo ya Ligi.

Kabla ya kusajiliwa na Young Africans, Kisinda alikuwa Mchezaji wa AS Vita Club ya kwao DR Congo.

Tuisila Kisinda (22) akiwa na RS Berkane katika Ligi Kuu ya Morocco 2021/22

23 Michezo.

01 Mabao.

04-Asssists.

Kwa mujibu wa Maghrib Foot, Uongozi wa RS Berkane umefikia makubaliano na TK Master ya Kuvunja Mkataba.

Name in home country: Tuisila Rossien Kisinda

Date of birth: December 20, 1999 (age 22 years), Kinshasa, Democratic Republic of the Congo

Citizenship: DR Congo DR Congo

Position: attack – Right Winger Foot: right.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live