Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Turpin Pilato Liverpool vs Real Madrid

Turpin Mwamuzi Clement Turpin

Thu, 12 May 2022 Chanzo: eatv.tv

Kamati ya waamuzi ya Shirikisho la soka barani ulaya UEFA imemteua muamuzi Clement Turpin (39) kuchezesha mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA Champions league 2022 kati ya Liverpool na Real Madrid.

Fainali hiyo itapigwa katika uwanja wa Stade de France mjini Saint-Denis, nchini Ufaransa jumamosi ya mei 28 mwaka huu kuanzi majira ya saa tatu usiku.

Turpin ambaye ni mwamuzi wa kimataifa tangu mwaka 2010, anatazamiwa kuchezesha fainali yake ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani ulaya akiwa mwamuzi wa kati baada ya kuhudumu akiwa Mwamuzi wa nakiba katika mchezo wa fainali ya mwaka 2018, ambao uliwakutanisha pia Real Madrid na Liverpool na Madrid kutwaa ubingwa kwa kushinda magoli 3 kwa 1.

Turpin amechezesha mechi saba ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu hadi katika hatua ya mtoano, ikijumuisha mchezo wa robo fainali ya kwanza kati ya Chelsea FC na Real Madrid katika dimba la stanford bridge jijini London.

Turpin pia ndiye aliyechezesha mchezo wa fainali ya ligi ya Europa msimu uliopita uliowakutanisha Villareal na Manchester United, na Villareal kutwaa ubingwa kwa mikwaju ya penati 11 kwa 10.

Chanzo: eatv.tv