Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunawapiga mapemaaaaa!

Mapemaa Pic Data Tunawapiga mapemaaaaa!

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Charles AbelMore by this Author SIMBA tayari ipo jijini Dodoma kwa mchezo wao wa kiporo cha Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, huku kila timu ikitamba itamaliza mambo mapema ili kuvuna pointi tatu na nyota wapya wa Msimbazi, Perfect Chikwende na Taddeo Lwanga wataionja ligi kwa mara ya kwanza.

Simba na Dodoma zitavaana kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma ikiwa ni kati ya mechi mbili za viporo zinazochezwa leo, nyingine ikipigwa Dar es Salaam kati ya KMC dhidi ya Namungo itakayopigwa Uwanja wa Uhuru.

Mechi hizo ni mwanzo wa kurejea upya kwa Ligi Kuu iliyosimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi 2021 na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji Wanaocheza Ardhi ya Nyumbani (Chan) zinazoendelea Cameroon.

Kusimamishwa kwa ligi hiyo kuliwafanya nyota wawili waliosajiliwa Sinmba dirisha dogo, Chikwende na Lwanga kushindwa kuanza kuitumikia, lakini leo wanaweza kuanza dhidi ya Dodoma kabla ya kuliwa kiporo kingine Jumapili Dar es Salaam dhidi ya Azam FC.

Kiwango bora kilichoonyeshwa na wawili hao katika mashindano ya Simba Super Cup yaliyofanyika wiki iliyopita na kile cha Lwanga kwenye Kombe la Mapinduzi, kinatoa ishara kuwa nyota hao watakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachoikabili Dodoma, huku wakihitaji ushindi zaidi kwa sababu kuu mbili.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz