Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunataka Mbappe, Neymar wakacheze Manungu?

Mbappe X Naymar Kylian Mbappe na Neymar

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Nimewahi kumsikia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mohammed Mchengerwa akizungumzia nia ya serikali kuona Tanzania inafuzu fainali za Kombe la Dunia 2030. Ni nia njema kabisa. Ni jambo jema kuona walau serikali ikiwa na nia ya kuona nchi inashiriki fainali hizo za Kombe la Dunia. Lakini tuko tayari kweli? Usinipe jibu.

Kutoka Afrika msimu huu timu zilizofuzu Kombe la Dunia kule Qatar ni Morocco, Cameroon, Tunisia, Ghana na Senegal. Kwa nafasi tano Afrika waliokosa ni pamoja na Misri ya Mohammed Salah, Ivory Coast ya Wilfred Zaha, Nigeria ya Kelechi Ihenacho na Algeria ya Riyad Mahrez. Hapo nimetaja tu nchi chache.

Hapo nimetaja tu baadhi ya wababe wa Afrika waliokosa fainali Qatar. Ni kweli Tanzania tuko tayari kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2030? Sidhani. Sioni dalili kama tumefika viwango. Sidhani hata kama tunajua sababu za timu kufuzu kwa Kombe la Dunia. Naiheshimu sana serikali. Nafurahi kuona walau sasa hata nia ipo, lakini bado hatujafika hata robo ya ndoto hizo. Kombe la Dunia sio michuano ya kila taifa. Tanzania bado hatuko eneo hilo.

Nchi yetu bado ina mambo mengi ya kujifunza kwa mataifa yaliyoendelea kwenye soka. Angalau kwanza tungekuwa tunafuzu mara kwa mara michuano ya Kombe la Afrika (Afcon) ili kujijengea uzoefu wa kuhimili vya kutosha michuano mikubwa zaidi ya soka yaani Kombe la Dunia.

Kumbuka tumeshiriki fainali za Afcon mara mbili tu katika historia ya nchi hii tangu tupate uhuru 1961.

Tulishiriki mara ya kwanza Nigeria 1980 kisha tukakaa miaka 39 na kushiriki mara ya pili 2019. Kama kufuzu Afcon ni mtihani mzito kwa Kombe la Dunia tunaweza na hata tukienda tutafanya maajabu gani?

Nilimsikia waziri wa michezo akizungumzia dhamira ya kufuzu Kombe la Dunia siku chache zilizopita.

Nimemsikia pia naibu katibu mkuu wa wizara hiyo akizungumzia wiki hii juu ya nia ya serikali kufuzu Kombe la Dunia 2030. Unadhani inawezekana? Sina jibu.

Mwaka huu baada ya kufuzu Cameroon, Morocco, Ghana, Senegal na Tunisia hata kelele sina kwa timu za Afrika. Nadhani serikali inatakiwa kutoa nafasi kwa wataalamu ili kuongeza pia thamani ya ligi.

Tatizo kubwa kila utawala unataka kuona nchi yetu tunafuzu Kombe la Dunia. Mafanikio wakati mwingine ni kama mbio za kupokezana vijiti. Hujui utafanikiwa lini. Tanzania bado hatuna uwezo wa kucheza Kombe la Dunia kwa sasa. Lazima tupate mahali pa kuanzia. Tatizo ni kwamba kila mtu anataka kuonekana shujaa kwa kuipeleka Taifa Stars Kombe la Dunia. Kiukweli naona dhamira ya serikali kutaka kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Kombe la Dunia sio kwamba tumejitahidi, ni kuonyesha heshima tu kwa wahusika, lakini mioyoni ni majanga matupu.

Watoto kwa mara ya kwanza wanataka kubaki na baba tu. Mazingira ya kupoteza mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia inaweza hata kuchangiwa na umasikini. Kupanga ni kuchagua. Uongozi huu unaweza kukuita kwenye ushiriki lakini uwezo wa kawaida.

Kila kiongozi anayekuja kwenye michezo anapambana. Kama tunataka Kombe la Dunia la haraka ni kumsubiri tufanye utofauti. Kama zimefuzu timu tano kwenda. Kama nchi ni lazima tuanze kwa kuweka vipaumbele. Kama tunaaanza na miundombinu tuwekeze vya kutosha. Kama ni kuanza ni kutengeneza kitu kwani kama tu Misri, Ivory Coast, Algeria na Nigeria hawana uhakika wa kucheza Kombe la Dunia za 2030, Tanzania tunatoa wapi huu ujasiri?

Kifupi ni kwamba bado hatujafanikiwa levo za kupasogelea. Kufuzu Kombe la Dunia sio masihara. Serikali bado haijawahi kufanya Bongo Fleva kuwa kipaumbele. Bado watu hawaamini kwenye kukuza vipaji. Ni kama kila mtu anaona wachezaji wa kigeni wako mbele ya wazawa. Watu kama kina Mwamnyeto hakusafiri tunakwenda naye.

Sina tatizo na serikali kila mtu kutaka tufuzu Kombe la Dunia lakini ningependa kuona waliopotea wanarudi. Misri, Ivory Coast, Algeria, Nigeria hawa wote hawajawahi kuwa na uhakika wa kushiriki finali za Dunia sembuse Tanzania?

Kama nchi tuna mambo mengi tunayopotezea kwa haraka zetu. Kama nchi kuna vitu tunavikimbia. Mwaka 2030 nadhani ni mapema sana. Tunaweza kuja kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia lakini sio kirahisi.

Ni ngumu kuweza kumpeleka Kylian Mbappe au Neymar na mastaa wengine wa dunia wakacheze Manungu au Jamhuri pale Morogoro? Ndio. Hatujawahi kuwa na viwanja bora na hata miundombinu na hata umeme wa uhakika wa kuweza kuvutia na kupewa uenyeji wa michuano mikubwa kama hiyo.

Morocco na Afrika ya Kusini wanaonekana kuwa na jambo. Nieleweke tunaweza kufuzu Kombe la Dunia lakini sio kwa haraka kiasi hicho. Ni lazima tujipange kwa muda mrefu kutengeneza timu itakayotuvusha na kutupa heshima kwenye michuano ya Afrika ikianza ile ya Chan tuliyowahi kushiriki mara mbili tu tangu michuano iasisiwe 2009. Kisha baada ya hapo tufanye mambo kwenye Afcon halafu ndipo tutaweza kwenda Kombe la Dunia. Naelewa nia ya serikali.

Chanzo: Mwanaspoti