Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tunamshusha tembo kesho kileleni - Ally Kamwe

Ally Kamwe Kijembe Tunamshusha tembo kesho kileleni - Ally Kamwe

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi Yanga SC wametamba kwamba kesho ndio siku yao ya kumshusha tembo kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Isikupe tabu licha ya kuwa hajaweka wazi kuhusu tembo ni nani lakini ni dhahiri shahiri, tembo atakuwa ni Simba SC ambaye ndiye yupo kileleni kwenye msimamo kwa sasa baada ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu.

"Kesho Wanayanga tujitokeze kwa wingi tunataka kumshusha tembo pale alipo ili sisi tukae mahali petu," alisema Kamwe.

Yanga wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wakiwa wamecheza mechi moja tu ya Ligi Kuu dhidi KMC na kuibuka na ushindi wa goli 5-0.

Kesho anakwenda tena kuzisaka alama tatu dhidi maafande wa JKT Tanzania ambao wamepanda Ligi Kuu msimu huu. Mechi yao ya kwanza dhidi ya Namungo, JKT walishinda kwa goli 1-0 wakiwa ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live