Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Tunahitaji umoja na mshikamano ili tufuzu"- Babra Gonzales

Babra Gonzalez Mtendaji mkuu wa Simba Sc, Babra Gonzales

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Babra Gonzales amesema wanahitaji kuungwa mkono kwa asilimia 100 kuelekea mchezo wao wa marudiano dhidi ya Jwaneng Galaxy ya nchini Botswana.

Akizungumza mara baada ya mchezo wao wa kwanza ambao Simba wameibuka na ushindi wa magoli 2-1, Babra amewapongeza wachezaji na benchi zima la ufundi lakini akasema wana kazi kubwa kuhakikisha wanalinda ushindi huo ili kufanikiwa malengo ya kufika mbali katika michuano hiyo.

"Kwanza tunamshukuru mwenyezi mungu kufikia hapa leo, tunawakilisha Watanzania wote,tumeshinda ugenini na sasa focus yetu ni mchezo wa nyumbani"

"Tunaomba wadau wa soka, Mashabiki, Wanahabari na watanzania wote wanaopenda mpira kutupa ushirikiano ili tukailetee sifa nchi" amesema Babra

Kwa sasa Simba inarejea kujiandaa na mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika Oktoba 24, saa 10: 00 katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo utahudhuriwa na Mashabiki 15000 pekee kwa ruhusa iliyotolewa na CAF, kupitia TFF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live