Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuna moyo wa kizalendo?

Simba X Yanga CAF Tuna moyo wa kizalendo?

Fri, 29 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama tungekuwa tunapendana kweli basi tungetamani kuona vilabu vyetu pendwa vya Simba SC na Yanga SC vikiombeana mema na kuungana mkono kwenye hii michezo yao mikubwa ya Klabu Bingwa Afrika. Kwangu najua ni ngumu.

Khalid Aucho anarejea wapo ambao wamefurahishwa na hii lakini wengine watakuwa wamehudhunishwa hawakutaka kuona urejeo wa Daktari Khalid Aucho.

Kwa Yanga SC hii ni habari njema tena inayofurahisha mashabiki wengi kwa hivi sasa, tunafahamu ubora wa kiungo huyu anapolikamatia dimba la chini (Central Midlfield) nini kinatokea, ni yeye kukaba na kusambaza upendo ambao unaifanya kazi ya wachezaji wengine wa Yanga kuwa rahisi.

Wengi wetu wanafurahishwa sana na aina ya soka ambalo linawafanya wengi kuvutika yaani kuvutiwa na burudani zaidi.

Aina ya uchezaji wa Aucho pengine unaweza usikufurahishe sana lakini ni moja ya wachezaji ambao wanajua kutimiza majukumu yao ipasavyo. Kukata mirija katikati ya uwanja, kuunganisha timu eneo la kiungo na ushambuliaji.

Nisiandike sana kubwa tusubiri Jumamosi itaenda kutoa Picha nzuri baada ya kurejea kwenye kikosi. Naamini kazini kwa Aucho kuna kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live