Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumuombee rais wetu- Samatta

611a79eaae162eb483a787c83cd00734 Tumuombee rais wetu- Samatta

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

NAHODHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta amesema Tanzania imepata pigo kubwa kufi wa na rais John Magufuli.

Aidha alisema kilichobaki ni kumuombea na kufanya mazuri aliyoyacha. Samatta, aliandika hayo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akiomboleza kifo cha rais wa awamu ya tano, Magufuli aliyefikwa na umauti juzi akisumbuliwa na tatizo la moyo.

“Pigo kwa taifa, Pigo kwa Tanzania tutakukumbuka daima kwa yote mazuri uliyoyapigania na kuyatekeleza katika vipindi vyako vya uwaziri na urais wa nchi yetu.

“Pole kwa mama Janet na familia,Pole kwa mama Samia nasi watanzania umeumaliza mwendo mzee wetu, tunakuombea upumzike kwa amani,” aliandika Samatta.

Nahodha wa kikosi cha Simba, John Bocco katika ukurasa wake wa Instagram aliandika: “Kweli kizuri hakidumu pumzika kwa amani mzalendo wa kweli, mtanzania ulieiweka Tanzania mbele na sio ubinafsi naamini wakujifunza tumejifunza mengi sana kutoka kwako na wakuona tumeona mengi sana mazuri kutoka kwako pumzika kwa amani Rais wangu.”

Nyota wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva, anayecheza soka nchini Moroco aliandika haya katika ukurasa wake wa Instagram “Pigo kubwa kwa taifa daima tutakukumbuka kwa yote mazuri uliyotufanyia siwezi kuyasema mangapi katika vipindi vyako vyote vya uwaziri na uraisi pole sana mama Janeth na family kwa ujumla!nenda mzee wetu tupo nyuma yako kwa maombi! Pumzika kwa amani rais wangu.

Kipa wa klabu ya Simba Aishi Manula naye aliandika haya katika ukurasa wake wa Instagram “Daaaaah hakika kwake tutarejea binafsi umetekeleza kile Mungu alitaka ufanye kwa watanzania na huna deni kwetu ulale mahala pema peponi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz