Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumpe Ally Kamwe maua yake kabla ya kifo chake

Ally Kamwe Mpira Ahmed Ally, Ofisa Habari wa Simba SC

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati tundu za pua za Ali kamwe zikizidiwa vyema na hewa nzito ya Benjamin mkapa stadium, bila shaka alikuwa akiendelea kupambania uhai wake dhidi ya adui anayekuja bila hata kugonga hodi, kifo.

Ni dhahiri vinyoleo vya mwili wake viliendelea kusisimka kila alipozidi kusikia kelele hafifu zilizopenya kwenye masikio yake huku matundu ya pua yalikuwa 'busy' kukinzana vyema na pumzi. zilikuwa kelele za ushindi na zilizobeba matumaini ya robo fainali.

Wananchi walijinadi na kujipiga vifua vyao. furaha ziliambatana na kila aina ya vicheko. Hii yote ilitokana na maonyesho ya burudani bora kwenye mboni za macho yao.

Ingekuwaje Pacome Day bila Pacome?Kwenye mahojiano dhidi ya Waandishi wa habari pale jangwani, Ali Kamwe alithibitisha kuumia kwa Pacome ni siku moja kabla ya mechi.

Licha ya maumivu makali ya nyama za paja. Pacome alitoa kauli kwa dokta ni lazima aanze. Ni kauli ambayo ilibeba moyo wa kishujaa kutokana na hamasa za Ali kamwe nje ya uwanja.

Pacome alitaka kuliacha jasho lake kwenye uwanja wa vita, hakujali maumivu yake ya nyama za paja, ubongo wake uliwawaza zaidi wale mashabiki wendawazimu waliozichafua nywele zao kwa ajiri yake. Watanielewa vipi? Huenda ndio swali lililokuwa linazunguka kwenye fikra zake.

Pacome alikubali kubeba maumivu kwenye miguu yake kwa sababu ya hamasa za wananchi. huenda ndio hamasa bora zaidi kufanywa na Ali kamwe. Alishinda moyo wa kijana kutoka Ivory Coast aliyeamua kubeba bendera ya jangwani kizalendo.

Ni wakati wa kumpa maua yake Ali kamwe, kabla binadamu hatujachagua kuwa wanafiki na kumpa maua yake baada ya kuvuta pumzi yake ya mwisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: