Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumesikitishwa fainali ya Yanga na Azam kuhamishwa - Gekul

Serikali Inatoa Haki Sawa Ushiriki Wa Michezo Gekul.jpeg Tumesikitishwa fainali ya Yanga na Azam kuhamishwa - Gekul

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Manyara mjini Pauline Gekul amesema wananchi wa Mkoa wa Manyara wamekuwa wakihoji kwanini mechi ya finali ya Kombe la Shirikisho la CRDB imeondolewa Mkoani Babati na kupelekwa Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

Gekul amesema kuwa wamewapa maumivu makubwa Wanababati kwa kuwaondolea finali hizo ambazo zimepangwa kufanyika Juni 2, 2024 kwa kigezo cha usalama.

Ameiomba Bodi ya Ligi Tanzania na TFF kuangalia upya namna ya kuwapunguzia machungu kwa kuwapa mashindano mengine yatakayochezwa kwenye uwanja wao ulioandaliwa kwa muda mrefu.

“Jana tumaini la Wanamanyara lilifia baada ya kusikia fainali hizi zimepelekwa sehemu nyingine naomba nieleweke wazi nimejifunza Watanzania wengi wetu tunaweza tukawa tunatengeneza maneno ambayo hata Mtu anakuwa hajasema.

"Sina tatizo mchezo huo kupelekwa popote tatizo langu ni moja Wanamanyara walivyojiandaa wakaenda re-allocate bajeti tukachukua fedha za Halmashauri, kwa Wadau tukawekeza Watu wamekopa Watu wameweka malikauli bidhaa tumaini lao limefifia.

"Mimi naelewa TFF walikuwa na nia nzuri kabisa mpaka jana timu yetu ya Mainjinia walikuwa uwanjani hali sio nzuri,” amesema Pauline Gekul.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live