Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumepewa wenyeji ufunguzi wa AFL sababu ya ubora wetu - Simba SC

Ahmed Ally Semaji La Simba.jpeg Tumepewa wenyeji ufunguzi wa AFL sababu ya ubora wetu - Simba SC

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC kupitia kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally, wamesema wamepata nafasi ya kuwa wenyeji wa ufunguzi wa Africa Football League kutokana na ubora wao.

Amewakataka Wanasimba, kujivunia jambo hilo na kutembea kifua mbele.

"Kuna jambo kubwa Afrika hii ambalo ni AFL linaihusisha Simba na Al Ahly. Ni heshima kubwa Simba tumepewa kuandaa mechi ya ufunguzi wa mashindano haya kwa mara ya kwanza."

"Wengine wataishi maisha ya shida sana wiki hii, na sisi sio shida zetu tutazidisha dozi."

"Tumepewa wenyeji wa michuano hii sababu ya ubora ambao tupo nao, zipo timu nyingi Tanzania, zipo timu nyingi Afrika lakini walikaa kujadili timu gani inafaa wakaona Simba Sports Club."

"Hatujapata nafasi hii kwa bahati mbaya, tumepata kwa ubora tulionao. Kama sio Simba kuwepo Tanzania basi Tanzania kusingekuwa na timu inayoshiriki African Football League kwa sababu baada ya Simba hakuna mwingine mwenye mafanikio kimataifa zaidi yetu."

"Ukweli unabaki kuwa sisi Wenye Nchi ndio tumeleta AFL hapa. Wanasimba mna nafasi kubwa ya kujipongeza, kufurahi sababu tumekomboa nchi kupata nafasi ya michuano hii, na kwenda mbali zaidi ya kuwa mwenyeji wa michuano."- Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live