Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumemuangusha Majogoro, Tukamuinua Mayele

Majogoro X Mayele Tumemuangusha Majogoro, Tukamuinua Mayele

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huyu ni Baraka Gamba Majogoro Baraka Gamba Majogoro Home boy anayekipiga pale Chippa United FC ya Bondeni kwa Madiba. Anakiwasha kwa uwezo wa hali ya Juu na wazulu wanamuimba ila hakuna anayejali hapa kwetu. Sisi tumezama kwenye Dimbwi la ushabiki na Sio Mustakabali wa Soka letu.

Pichani mkononi kashika Tuzo ya Mchezaji vora wa mechi "Man Of The Match" kwenye mechi dhidi ya Super Sports united. Huku kwetu haikua habari kubwa, imepita wiki ya pili sio habari kubwa wala hakuna anayeimba jina la BARAKA GAMBA MAJOGORO.

Sasa jana Fiston Kalala Mayele kashinda "Man Of The Match" imekua habari kubwa saaana huku kwetu, kila mtu anaandika kuhusu Mayele kuwa kawa mchezaji bora wa Mechi. Nauliza kwa Maslahi ya nani? Yaani vijana wetu wetu wanafaidika nini na habari hii kuliko ya kijana wetu Baraka Gamba?

Tupo katika dimbwi la utumwa, tupo katika dimbwi la ujinga tusioujua, Sio kama namchukia Fiston Mayele, hapana bali nachukia namna tunampa thamani mbele ya wazawa. Wote wanacheza ligi nzuri Afrika, huyu mzawa alitakiwa apaziwe sauti sababu ya hamasa kwa vijana wetu.

Hatuwapendi Wazawa, Hatuwaombei kheri, tunawapa Thamani wageni hata wakiondoka, hii ni KANSA inayokula morali ya vijana wetu. Baraka alipaswa kuwa hamasa kwa kila kijana ambaye ndoto yake ya kutoka nje imekua lazima afika Yanga au Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live