Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumejifunza, mwakani tutakuwa vizuri - Power Dynamos

Msg Power.jpeg Tumejifunza, mwakani tutakuwa vizuri - Power Dynamos

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Power Dynamos, Chipepo Mwenya amesema kuwa wamejifunza kutokana na makosa waliyoyafanya kwenye michezo miwili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ya SImba SC ya Tanzania.

Chipepo amesema hayo jana mara baada ya kutoka sare na Simba ambao wamefanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya bao 3-3.

"Tumehuzunika kupoteza mchezo huu, sababu tulikuja hapa kwa ajili ya kushinda na kutinga hatua ya makundi ya CAFCL baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa muda mrefu. Lakini tumejifunga wenyewe jambo ambalo limetuumiza sana.

“Siwezi kuzungumzia marefa, nao ni binadamu wana mafanya makossa kama wanadamu wengine, tumepoteza na hata kama nikizungumzia marefa tayari matokeo yatabaki vilevile.

“Nachoweza kusema ni kwamba tumejifunza vitu vingi kwenye mashindano haya, tumepoteza nafasi nyingi, hatukuzuia vizuri nab ado tumejifunga wenyewe.

"Tunaweza kuchukuziwa na matokeo haya, lakini kuanzia msimu ujao tutakuwa tumejua wapi pa kuanzia. Tumecheza mchezo mzuri kule nyumbani na wote mliona lakini kwa sababu ya kupoteza nafasi, tulihuzunishwa sana na hilo," amesema Chipepo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live