Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumechagua kuwadharau Azam FC?

Azam Kuendelea Na Mwendo Wa 5 0 Leo Tumechagua kuwadharau Azam FC?

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Youssouf Dabo kocha bishoo ana waongoza vijana Mafundi kucheza kandanda safi pale Chamazi Complex.

Alicho nivutia zaidi ni kumfanya Sospeter Bajana kuwa fundi zaidi, Lusajo Mwaikenda kuwa mtamu zaidi anapoenda kushambulia.

Kutengeneza mawinga wawili ambao wamekuwa mwiba Kwa walinzi wa timu pinzani Sillah na Kipre JRwamekuwa balaaa mabao mengi ya Azam FC yanapikwa huku.

Kipre JR chini ya Dabo amekuwa hatari wakati hapo awali alikuwa mchachari, misimamo yake na kupenda wachezaji wawe na nidhamu kumeifanya timu yake iwe bora sana ndani ya pitch.

Azam FC ya sasa yoyote anakufunga Kwa sababu inacheza kitimu zaidi bila kumtegemea mtu mmoja mmoja.

Azam ndiyo wanaongoza Ligi kwa sasa wakiwa na alama 25 wakiwa wamecheza mechi 11 na leo watacheza mchezo wa 12, Yanga wana alama 24 wakiwa wamecheza michezo 9 na Simba wana alama 19 wakiwa wamecheza michezo 8.

Hivi tuite Pira Dabo ama Pira Bruno Ferry?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live