Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tulliambiwa tuchague fidia au tujenge uwanja - Hersi

Hersiii 70000 Tulliambiwa tuchague fidia au tujenge uwanja - Hersi

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuhusu mipango ya kujenga uwanja wao wa kisasa katika eneo la Jangwani, walipewa machaguo mawili -- walipwe fidia na kuhama katika eneo hilo ambalo liko katika mipango ya kuboreshwa au wajenge uwanja ulio bora kabisa. 

"Serikali ilitufanya tuchague mambo mawili, kuachia uwanja ili turudishiwe fidia ama kujenga uwanja wa kisasa utakaoendana na eneo hilo, tulichagua namba mbili na sasa naamini Yanga itakuwa na uwanja wa kisasa hapa nchini."

"Tunamshukuru mzee wetu aliyetangulia mbele ya haki, Abeid Amani Karume aliyejenga jengo hilo mwaka 1971, lakini kila kitu kinatakiwa kufanyiwa marekebisho na sasa Yanga ndio iliyo na jengo la kisasa kuliko klabu zote Tanzania na kama siyo Afrika.

Mbali na hilo, alizungumzia msimu ujao (2024/25), kwamba watakuwa na msimu bora kuliko uliopita.

"Msimu bora unaanzia na usajili, tutakuwa na benchi bora kuliko la msimu uliopita, tutakuwa na wachezaji bora, kila mwaka tutaongeza wachezaji wenye ari na mafanikio, hatuwezi kubweteka kutokana na mafanikio tuliyopata, tutakuwa na kambi nzuri, tumealikwa Iran, Afrika Kusini na Kenya kufungua uwanja wao mpya wa kisasa," alisema.

Kwa kauli ya rais wa Yanga ni kama inakoleza moto wa kocha wao Muargentina, Miguel Gamondi ambaye bado hajasaini mkataba mpya na tetesi nyingi zinamzunguka ikiwamo kutakiwa na klabu nyingine.

YANGA PRINCES

Aidha, Injinia Hersi amesema japokuwa timu yao ya wanawake (Yanga Princess), haifanyi vizuri, lakini imefungua milango kwa mabinti kwenda kucheza nje ya nchi.

Alisema wanajipanga upya kuhakikisha timu hiyo itaanza kufanya vizuri na kuchukua mataji ya Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL), kwani tangu ainze kucheza ligi hiyo haijawahi kuchukua taji.

"Mfano Clara Luvanga anacheza timu ya wanawake ya Al-Nassr ya Saudia, Grace anacheza timu ya Uturuki, Maimuna Kaimu anacheza timu ya Misri, (Aisha Masaka yuko Sweden), hao ni baadhi tu ya wachezaji ambao wametoka Yanga Princes," alisema Injinia Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live