Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Tulitaka kuweka historia, ushindi dhidi ya Man United" - Salah

Salah Hat Trick Mohammed Salah akiwa na Klopp

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Liverpool,Mohamed Salah amefichua kuwa Liverpool ilitaka 'kuweka historia' katika mchezo wao dhidi ya Man United.

Mohamed Salah amekiri kwamba ndani ya vumba vya kubadilishia nguo hawakuwa na chembe ya huruma dhidi ya Manchester United wakati walipokwenda mapumziko katika mchezo ambao uliisha kwa Liver kuibuka na ushundi wa magoli 5-0.

Liverpool walikuwa mbele kwa magoli manne hadi mapumziko, Salah akitengeneza bao la kwanza la Naby Keita kabla ya kufunga mabao yake mawili, na akakamilisha hat-trick yake dakika chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Meneja wa Liver, Jurgen Klopp alikiri baada ya mchezo huo kuwa alimhurumia Ole Gunnar Solskjaer.

"Wakati wa mapumziko tulikuwa tunazungumza vyumbani kwamba tunahitaji kuandika historia, tunatakiwa kuendelea na kufunga mabao, tujaribu kufunga kadiri tuwezavyo," alisema (kupitia tovuti rasmi ya klabu).

"Nafasi kama hii haipatikani mara kwa mara. Kwa hivyo tulijaribu kufanya kila tuwezalo kushinda mchezo huo. Tulijua kabla ya mchezo itakuwa mechi ngumu ikiwa tunataka kushinda mchezo, ndivyo tulifanya. "

Bao la Salah dakika chache baada ya mapumziko lilihakikisha Liverpool wanatengeneza rekodi chache kwenye mechi hii. Kilikuwa ni kipigo kizito zaidi kwa United kuwahi kufungwa nyumbani na Reds, na mara ya kwanza kufungwa mabao matano bila wao kupata bao tangu 1955.

"Tangu mwanzo wa msimu tulijaribu kushinda kila mchezo. Tunacheza tu kwa ajili ya ubingwa kwa sababu timu kama Liverpool, wachezaji kama hawa, meneja kama huyu, tunahitaji kucheza ili kushinda kila kitu..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live