Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tulikata moto baada ya kufungwa la tatu na Raja-Ahmed Ally

AHMED ALLY MSEMAJI SIMBA Tulikata moto baada ya kufungwa la tatu na Raja-Ahmed Ally

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, kwenye mechi yao ya pili ya Hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa walikata moto baada ya kufungwa goli la tatu na Raja Casablanca.

Ahmed alisema, siku hiyo alikuwa hafatilii mechi bali zaidi alikuwa akiangalia jinsi ambavyo mashabiki wanashangilia kabla na hata baada ya kufungwa.

"Ukweli ni kwamba Raja hatuwawezi kwa kushangilia lakini siku ile walibebwa zaidi na ushindi wao, laiti tungewafunga sisi, wale wangeloa lakini bahati mbaya walipotufunga wao ndipo na sisi tukakata moto hasa baada ya kufungwa goli la tatu," alisema Ahmed.

Simba wanatarajia kuwakaribisha Vipers SC Marchi 7, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ikiwa ni mchezo wa marudiano baada ya wa awali kushinda 1-0 ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live