Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tukiwapiga Niger ni mwanga kuelekea Morocco

Taifa Stars AFCON.jpeg Tukiwapiga Niger ni mwanga kuelekea Morocco

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inaendelea na kambi yake ya maandilizi kwa ajili ya michezo yake miwili ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026.

Tanzania itacheza dhidi ya Niger utachezwa Novemba 18, 2023 kwenye mji wa Marrakech, Morocco na mchezo wa pili utakuwa nyumbani [Benjamin Mkapa Stadium] dhidi ya Morocco utachezwa Novemba 21, 2023.

Simon Msuva tayari amewasili kambini na amesema wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mechi hizo mbili huku wakiendelea na maandalizi.

“Kucheza timu ya Taifa ni kitu cha kujivuia, unapoitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ni heshima, tupo hapa kwa ajili ya kupambania taifa letu.”

“Niger ni timu ambayo tumeshakutananayo mara mbili kwa siku za hivi karibuni, mara ya mwisho tulichezanao hapa nyumbani na tukawafunga goli 1-0.”

“Tunaamini mechi haitakuwa nyepesi lakini tunaendelea kujiandaa vya kutosha kuipigania nchi yetu, kila mtu anajua umuhimu wa hizi mechi mbili lakini mechi dhidi ya Niger itatupa mwanga kuelekea mechi dhidi ya Morocco.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live