Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tukimpa 'thank you' mchezaji moubwa, Wanasimba msishangae - Ahmed

Realclatouschama Clatous Chama

Sun, 19 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba wamedhamiria kufanya usajili wa nguvu na kuwaondoa wachezaji wao ambao wanaonekana kutoisaidia timu hiyo ambayo imekosa taji la Ligi Kuu kwa msimu wa tatu sasa.

Miongozi mwa mastaa wanaotajwa huenda wakaachwa na Simba baada ya msimu huu kumalizika ni pamoja na viungo Clatous Chama, Saido Ntibazonkiza na Henock Inonga.

"Wanasimba wawe ‘Stand by’ kwasababu kuna watu ambao tutaachana nao lengo ni kuleta wengine. Kama kuna mchezaji unamuona bora na anaagwa basi usishtuke ujue anakuja mwingine bora zaidi, Tunachokihitaji ni kuboresha timu yetu na mchakato umeshaanza,” amesema Ahmed Ally - Meneja wa Idara ya Habari ndani ya klabu ya Simba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live