Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tukiendelea kubaki na wachezaji hawa, tutakufa kiume kila siku - Kiemba

Tukiendelea Kubaki Na Wachezaji Hawa, Tutakufa Kiume Kila Siku   Kiemba Tukiendelea kubaki na wachezaji hawa, tutakufa kiume kila siku - Kiemba

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Amri Kiemba, ameuchambua mchezo wa Simba dhidi ya Al Ahly na kusema, kuna wachezaji wanahitajika kuongezwa ili Simba iweze kufika hatua kubwa Kimataifa.

Kiemba ameyasema hayo mara baada ya mchezo huo kukamilika hapo jana Oktoba 24, 2023 na Simba kuondoshwa kwenye mashindano ya Afrika Footbal League kwa faida ya goli la ugenini.

“Ukiangalia michuano hii kuna kitu cha kijifunza, ukitaka kuchukua ubingwa wa Champions League hizi ndio timu ambazo zinashindana kupambania ubingwa.

“Kwa hiyo ukiangalia daraja la Ahly, Mamelodi, Esperance utagundua tumesogea lakini tunahitaji kuanza kuingiza daraja la wachezaji washindani wa daraja la Al Ahly.

“Kama tutaongeza daraja kidogo tunaweza kushindana, ndoto ya Klabu nyingi ni kufika Nusu Fainali na kwenda kuchukua ubingwa lakini kama tutaendelea kuwa na wachezaji wa madaraja haya kila wakati tutasema tumekufa kiume.

“Tukiangalia tulipotoka ni kweli tunasogea tunachohitaji kuongeza ni madaraja ya wachezaji wanaoshindana ndani ya uwanja kwa sababu ukiangalia jana kama ingekuwa tuna daraja tofauti na hili tunengeweza kuamua kwa sababu tumepata goli tungechukua muda kukaa na mpira.

“Lakini baada ya kupata goli ni kama Ahly walibadilisha gia ikawa ngumu kwa upande wetu na hata Dar es Salaam ilikuwa hivyo,” amesema Amri Kiemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live