Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tujikumbushe ya Nabi tujiulize ya Gamondi

Nabi Gamondi 2 WA0002 Tujikumbushe ya Nabi turejee ya Gamondi

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Nassredine Nabi alijiunga na Yanga wakati msimu wa 2020/2021 ukiwa unakaribia kufika ukingoni, akapata nafasi ya kukifanyia tathmini kikosi cha Wananchi, akapata nafasi pia ya kuendekaza baadhi ya sajili, na akapata wachezaji bora wakiwemo akina Fiston Mayele, Yanick Bangala, Djuma Shaban n.k, akauanza msimu akiwa na wakali hao.

Katika msimu huo Nassredine Nabi akakutana akatolewa hatua ya awali kabisa ya Klabu bingwa Afrika na Rivers United, akapewa muda wa kuinoa Yanga akiwa na mashindano ya ndani pekee na mwisho wa msimu akafanikiwa kutwaa Mataji ya ndani.

Msimu wake wa mwisho aliondolewa na Al Hilal katika Klabu bingwa licha ya maboresho kadhaa ya kikosi,lakini akapewa nafasi,akaipeleka Yanga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Nabi aliondoka na nyota kadhaa ambao walikua uti wa mgongo wa Klabu pia wakatimka Yanga, akaingia Miguel Gamondi, akapata maingizo mapya zaidi ya saba.

Amekutana na mashindano makubwa mapema kabisa na akaipelekea timu makundi ya Klabu Bingwa Barani Afrika baada ya miaka 25, alifanya usajili takribani wachezaji 7 ingawa wapo wachezaji ambao bado hawajaingia katika mzunguko wa uchezaji.

Ndio kwanza hata nusu msimu hajamaliza, watu wameanza kuhoji Gamondi anaua vipaji vya wachezaji, mara kwa nini hafanyi rotation kama Nassredine Nabi, swali ni je Gamondi amepata muda upi wa kukaa na kikosi kiasi cha kudhani anaweza kufanya kama iliyokuwa kwa Nassredine Nabi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live