Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuitazame Yanga vs Singida FG kimbinu zaidi

Skudu 4630735 Yanga vs Singida FG.

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naaaam! Ilikuwa ni mechi safi, mechi haina mbambambaa mechi ya ufundi mechi ya magoli burudani bul bul kwa wahusika na wasiohusika.

Twende pamoja

1.Timu zotee zikiingia kwa mfumo wa 4-2-3-1 kila timu ikitumia viungo wawili wa kati Singida FG wakiwatumia Yusuph Kagoma na Aziz Amdambwile, na Yanga wakiwatumia Zawadi Mauya na Mudathir Yahya.

2. Mechi ilikuwa ya kasi kwanini, pembeni ambapo mashambulizi ya timu zote yalikuwa yanaanzia palikuwa na watu ambao asili yao ni ukimbiaji kuanzia kwenye buid up nikimaanisha mabeki wa pembeni wenye kasi Kelvin Kijili na Yao Attohoula.

3. Beki za kati za Singida FG zilikuwa za moto sana kwenye kushinda mipira ya juu, kufanya tackling na clearence kusafisha mipira, yule Mackame ni Beki haswa one Vs one ilikuwa kazi ndogo sana kwake (muulizeni KONKONI)

4. Eneo la ushambuliaji la Yanga liliongozwa na Konkoni huku nyuma yake kukiwa na viungo washambuliaji watatu pure number 10 asilia (aziz, max na pacome) lilikuwa la moto sana kutokana na wote watatu kuwa na uwezo wa kupiga mashuti makali na ndilo eneo lililozaa magoli yote mawili yaliyofungwa na Maxi Nzengeli.

5. kwanini mechi ilionekana ikitembea sana? kwasababu kulikuwa na uwiano sawa hasa eneo la viungo hivyo kuruhusu open play iliyoacha eneo kubwa la kumuwezesha kila mtu kukokota na kugawa mipira hivyo viungo wote kuonekana kuwaka.

Mengineyo Aziz Ki mchezo ulimkataa, alionekana kuandamwa na fatigue (uchovu) pia leo man to man na one against one battle ilikuwa kubwa sana kwake.

Bruno Gomez bado hajarudi katika kiwango tulichokizoea, hayupo locomotive tena kama alivyokuwa ana kazi kubwa sana ya kufanya nje ya uwanja. Mashambulizi yalikuwa machache kwa upande wa Yanga Diara alibaki na usalama mkubwa sana.

Rotation ya kikosi cha Yanga ilikuwa kubwa sana, na wote walionekana kuwa na fitness ya hali ya juu sana.

UFUNDI Huyu Yahya Mbegu ni moto mwingine mtulivu sana, pasi sahihi na utundu wa mpira mguuni. Kelvin Kijili, silaha yake kubwa ni kasi akikutoka imeisha hiyo???? Shooting Stability ya Maxi Nzengeli ni exceptional muulizeni goal keeper wa Singida FG.

SKUDU MAKUDUBELA what a player amekataa kudharauliwa amekataa kusemwa ni kiumbe cha hatari sana, dribbling and ball driving yake vyenga na kuaibisha ilikuwa kazi yake pia kwa kutoa krosi yupo vizuri sana Kudos ???? Deus Kaseke, kakataa kuzeeka sina kumbukumbu yake ya kupoteza mpira leo alipokuwa uwanjani.

Zawadi Mauya, wow! watu walimsahau Aucho kwa muda, kafanya kazi zote zinazotakiwa, hapoi, haboi, pamoja na Yusuph Kagoma japo ni mrahisi kwenye kucheza madhambi ila alikuwa ndo engine ya Singida FG. Yao Yao weeh kama kawaida.

Goal keeper wa namba tatu wa Singida PARAPANDA ilikataa kulia, anajiamini sana akikuwa ana kitu atafika mbali.

WAAMUZI Walikuwa kwenye kiwango bora, hawakuifanya mechi kuwa rahisi aliruhusu. watu kugongana sana miili hivyo kama ni makosa basi ni yale yenye uzito tu yalikuwa faulo. Goal la Aziz ki halikuwa off-side all in all twende kazi punda afe mzigo ufike.

HITIMISHO Yanga wamechukua point tatu tena juu kileleni hongera kwao, Mchezo umeisha Yanga 2 - SingidaFG 0 huku mfungaji akiwa Max Nzengeli kwa magoli yote mawili pasi za magoli zikitoka kwa Pacome na Yao.

Walisubiria SKUDU acheze vibaya ili wapone kovu la ONANA ETOO kula chuma hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: