Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuisila Kisinda Atuma Salamu Yanga

Tuisila One Tuisila Kisinda

Fri, 4 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ALIYEKUWA winga wa Yanga, Tuisila Kisinda, amefunguka kufurahishwa na klabu yake ya zamani kuongoza ligi kwa alama nyingi dhidi ya Simba huku akiweka wazi kuwa matamanio yake ni kuiona Yanga ikitwaa ubingwa msimu huu.

Kisinda ambaye amedumu kwa msimu mmoja pekee ndani ya Yanga, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco inayonolewa na kocha Florent Ibenge.

Kisinda alisema kuwa anajisikia furaha kuona timu yake ya awali ikiwa inafanya vizuri katika msimamo wa ligi kuu huku akiweka wazi kuwa anatamani kuona timu hiyo ikitwaa ubingwa msimu huu mara baada ya msimu uliopita kuukosa.

“Nafurahi kuiona Yanga ikiwa inaongoza mbele ya Simba tena kwa pointi nyingi, msimu uliopita ubingwa haukuwa kwa Yanga lakini kwa hiki ambacho kinaendelea kwa sasa ni dalili nzuri za ubingwa.

“Mimi napenda kuiona Yanga ikifanikiwa mara baada ya kushindwa kutwaa kwa muda mrefu ubingwa wa ligi kuu, hivyo nitafurahi kama ndoto hizo zitakamilika kwa Wanayanga kufurahia ubingwa wao,” alisema mshambuliaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live