Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuisila, Bocco wazidiwa ujanja

Bocco Pic Data Tuisila, Bocco wazidiwa ujanja

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

JOHN Bocco anaongoza orodha ya mabao Ligi Kuu Bara sambamba na Meddie Kagere, lakini nahodha huyo wa Simba na winga teleza wa Yanga, Tuisila Kisinda wamezidiwa ujanja kwenye upigaji penalti katika ligi hiyo mpaka sasa ligi ikiwa imesimama.

Kama hujui, mpaka sasa Ligi Kuu ikiwa raundi ya 24, tayari penalti 30 zimepigwa na Bocco, Tuisila, Chris Mugalu, Clatous Chama na Deus Kaseke, mastaa wa Simba na Yanga ni miongoni mwa waliokosa mikwaju yao na kuzinyima timu zao pointi na mabao kwenye mechi zao.

Katika penalti hizo 30, Marcel Kaheza wa Polisi Tanzania na Lenny Kissu wa Biashara United ndio vinara wa kutupia kambani mikwaju hiyo, huku Azam FC ikiwa imeshababisha penalti nyingi zaidi mpaka sasa, ikifuatiwa na KMC, Tanzania Prisons na Dodoma Jiji.

Kaheza mwenye mabao matano katika wafungaji, amepiga penalti tatu mpaka sasa na zote ametupia kambani, akiifukuzia rekodi ya Peter Mapunda aliyekuwa Mbeya City msimu uliopita aliyeongoza kwa kufunga penalti saba katika mabao yake 13 ndani ya VPL 2019-2020.

Mapunda kwa sasa anakipiga Dodoma Jiji na mpaka sasa amefunga bao moja tu, baada ya kutumia dakika kibao bila kucheka na nyavu.

Kaheza alifunga dhidi ya Prisons, Dodoma Jiji na JKT Tanzania, akifuatiwa na Kissu, beki aliyepiga penalti tatu na kufunga mbili dhidi ya Dodoma Jiji na KMC na kupoteza moja dhidi ya Azam FC.

Pia kuna watano waliowafutia Kaheza na Kissu, wakipiga mbili mbili, lakini kila mmoja aliambulia moja tu, Bocco aliyefunga dhidi ya Kagera Sugar na kukosa dhidi ya Ruvu Shooting na Tuisila aliyefunga dhidi ya KMC na kukosa kwa Wagosi wa Kaya.

Wengine ni Bigirimana Blaise (Namungo) alipata dhidi ya JKT Tanzania na kukosa dhidi ya Yanga, Yusuf Dunia (Gwambina) alifunga dhidi ya Mtibwa ila akakosa dhidi ya Coastal Union na Salum Kihimbwa wa Mtibwa Sugar aliyefunga dhidi ya Namungo akakosa kwa Dodoma Jiji.

Azam imepata penalti nne, mbili ikifungwa na mbili timu pinzani zikikosa. Timu hiyo ilipigiwa penalti dhidi ya Biashara iliyofungwa na Kissu alikosa na dhidi ya Simba, Clatous Chama alikosa.

Azam iliendelea kusababisha penalti katika mchezo na Coastal na Haji Ugando alifunga kama ilivyo kwa Peter Mwalyanzi wa Kagera Sugar aliyefunga pia dhidi yao na timu inayoifuata ni KMC, Prisons na Dodoma Jiji zilizopigiwa penalti tatu kila moja.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz