Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuhuma za kuuza mechi zimewaathiri wachezaji Simba - Mwakisu

Tuhuma Za Kuuza Mechi Zimewaathiri Wachezaji Simba   Mwakisu Tuhuma za kuuza mechi zimewaathiri wachezaji Simba - Mwakisu

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Musa Mwakisu amesema, kashfa ya baadhi ya wachezaji kudaiwa kuuza mechi imewasababisha wachezaji wa Simba SC kucheza chini ya kiwango dhidi ya Namungo FC.

Simba waliokuwa wenyeji kwenye mchezo wa raundi ya tisa ya Ligi Kuu ya NBC, walilazimika kupata sare ya 1-1 baada kutanguliwa kufungwa.

"Wachezaji walikuwa na siku mbaya sana mchezoni jana, ni kama vile walikuwa wameathiriwa kisaikolojia na suala la kuuza mechi dhidi ya Yanga, mchezo wa mpira unachezwa kuanzia kichwani, wao hawakuwa sawa," alisema Mwakisu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live