Kocha wa Bayarn Munich, Thomas Tuchel inaelezwa yupo kwenye mpango wa kutua Barcelona dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuondoka Bayern ili akachukue nafasi ya Xavi.
Tuchel ambaye ataondoka Bayern mwisho wa msimu huu baada ya kufanya makubaliano na vigogo wa timu hiyo, amekuwa akihusishwa na timu mbalimbali ikiwamo Manchester United na kwenye orodha ya makocha wanaotakiwa na miamba hiyo ya Old Trafford, yupo pia Zinedine Zidane, Julen Lopetegui na Graham Potter na Tuchel ndiye anapewa nafasi kubwa ya kutua Barca.
Hata hivyo, taarifa kutoka Hispania zinasema Barca imetuma maombi ya kumtaka kocha huyo asiondoke mwisho wa msimu, sababu kubwa ikitajwa ni miamba hiyo imekuwa ikipitia kipindi kigumu kwenye kumpata kocha mpya na makocha wengi wakubwa wamekuwa wakikataa ofa zao.
Xavi aliweka wazi ataondoka kwa miamba hiyo ya Nou Camp mwisho wa msimu, mkataba wake unamalizika mwaka na Barca wanahitaji aendelee kuwepo.
Barca imekuwa ikikimbiwa na makocha kwa kile kinachoelezwa wengi wanaona itakuwa ngumu kufanikiwa kwa sababu ya hali ya kiuchumi ya timu hiyo kuwa ni mbaya.
Tuchel anaonekana kuwa mbadala sahihi Bayern ingawa naye anadaiwa kuwa na chaguo lake la kwanza na amepanga kutua Man United na kama mambo yakifeli ndio anaweza kufikiria kujiunga na Barca.