Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuchel awakomalia Werner, Ziyech

Tuchel Werner Ziyechi Hakim Ziyech akiwa Timo Werner

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Chelsea Thomas Tuchel ameripotiwa kuweka msimamo kwamba sio Timo Werner wala Hakim Ziyech atakaeondoka anaondoka Stamford Bridge wakati wa dirisha la usajili la mwezi Januari.

Barcelona wamehusishwa zaidi na wachezaji hawa wote wawili, huku miamba hao wa Catalan wakiwa wana jaribu kuimarisha safu yao ya ushambuliaji mwanzoni mwa 2022 kwa usajili wa mkopo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Sport, timu ya Xavi imefahamishwa kwamba hakuna mchezaji wa Chelsea atakayepatikana katikati ya kampeni ya 2021-22.

taarifa hiyo inadai kuwa Tuchel anataka kuwaweka pamoja kuwa sehemu kubwa ya kikosi chake cha kwanza kwa msimu mzima, huku The Blues wakipania kuwania taji la Ligi Kuu na taji la Ligi ya Mabingwa.

Werner amefunga mara tatu na kutoa asisti moja kwenye mechi 12 alizoichezea Chelsea msimu huu.

Ziyech, ambaye alihusishwa sana na kutaka kuondoka Stamford Bridge msimu wa joto, amecheka na nyavu mara tatu na kutoa asisti nne katika mechi 15 za ugenini kwa mashindano yote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live