Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuchel atajwa kurithi mikoba ya Southgate

Tuchel X Southgate Tuchel atajwa kurithi mikoba ya Southgate

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kocha wa England Gareth Southgate kutangazwa kwamba amejiuzuru kuifundisha timu hiyo juzi, baada ya kuhudumu kwa karibia miaka nane, taarifa zinaeleza kocha wa zamani wa Chelsea, Bayern Munich na Borussia Dortmund Thomas Tuchel huenda akachaguliwa kuwa kocha mpya wa England ikiwa Gareth Southgate atajiuzuru.

Hii inakuwa ni mara yapili kwa Tuchel kuhusishwa na kibarua hiki kwani iliwahi kuwa hivyo mwaka 2022 baada ya Southgate kufanya vibaya katika Kombe la Dunia lakini ilishindikana kumpata na mwisho mabosi wa FA ya England wakaamua kumuongeza mkataba Southgate uliokuwa unatarajiwa kumalizika Desemba mwaka huu.

Southgate amejiuzuru baada ya kupoteza fainali dhidi ya Hispania kwa mabao 2-1 ambayo ilikuwa ni fainali yake yapili akiwa na England tangu alipochukua mikoba ya kuifundisha Novemba 2016.

Akithibitisha kuondoka kwake jana Southgate alisema: "Kama Muingereza imekuwa fahari na heshima kwangu kucheza na kuifundisha timu ya taifa ya England, hii ina maana kubwa kwangu na nilijitolea kila ktu changu, lakini umefika muda wa mabadiliko na kuingia kwa a sura mpya. "

Mbali ya kufika fainali ya Euro mara mbili mfululizo, kocha huyu pia alifanya vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 alipomaliza nafasi ya nne, pia mwaka 2022 alipowezesha timu hiyo kufika robo fainali.

Katika kipindi chote alichohudumu, Southgate aliiongoza England katika mechi 102m akashinda 64, sare 20 na kupoteza 18.

Taarifa za kuondoka kwa kocha huyu zilianza kusambaa tangu wiki iliyopita na mara baada ya kupoteza fainali kauli zake zilitafsiriwa kwamba ni mtu anayetarajia kuondoka.

Kupitia taarifa iliyotolewa na The Sun inafafanua kwamaa wakati anazungumza baada ya kupoteza fainali alisema alisema: "Nadhani England wako katika nafasi nzuri sana kutokana na wachezaji waliopo kuwa na uzoefu wa michuano kama hii, ukiangalia pia umri wa wachezaji wengi watakuwepo katika michuamo ya Kombe la Dunia na Euro ijayo pia."

Alionyesha kuwa kazi yake imefikisha mwisho na sasa ni muda wa England kusonga mbele.

Tuchel kwa sasa yupo huru baada ya kuvunjiwa mkataba na Bayern mwisho wa msimu uliopita.

Mabosi wa FA ya England wanamwangalia kwa jicho lapili kwa sababu amefanya vizuri karibia timu zote alizozifundisha ambapo kwa ujumla ameshinda mataji makubwa kama Ligi ya Mabingwa, Bundesliga na Ligue 1.

Mbali ya Tuchel, kocha mwingine ni Eddie Howe kutoka Newcastle ambaye aliwahi kusema kwamba ana ndoto ya kuifundisha timu hiyo ya taifa siku moja.

Hata hivyo kwa Eddie inaonekana kuwa ngumu kwa Newcastle kukubali kumruhusu kwa sasa.

Mauricio Pochettino ambaye naye hana kazi tangu aachane na Chelsea katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu.

Ikiwa watashindwa kuwapata makocha tajwa hapo juu, FA ya England inaweza kumpandisha kocha wa timu ya vijana wenye umi wa chini ya miaka 21, Lee Carsley na kumpa majukumu hayo mazito.

Chanzo: Mwanaspoti