Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuchel alalamikia Corona

Tt Chelsea Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amesema kuwa usalama wa wachezaji uko hatarini kwa sababu timu yake ililazimika kucheza mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Wolves huku baadhi ya wachezaji wakiwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19.

Kikosi cha Chelsea kimeondoka na alama moja baada ya sare tasa dhidi ya Wolves ambayo ni mbaya kwenye mbio za kuwania ubingwa katika mchezo dhidi ya Wolves uliopigwa Molineux leo Jumapili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumalizika kwa mchezo na sare tasa kuzaliwa, kocha Tuchel amesema “siyo salama hata kidogo”, alisema.

“Tumekuwa tukizungumza namna ya kuwalinda wachezaji na mazingira rafiki lakini usalama huo haupo, siwezi kushangaa kuona mechi ijayo tukiwa na idadi chanya nyingi zaidi”.

Mechi sita za Ligi Kuu England zilipigwa chini wikiendi hii kutokana na virusi vya Covid-19, moja ya mechi hiyo ni ya Aston Villa na Burnley, mchezo ulioahirishwa masaa mawili kabla ya mchezo huo kuanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live