Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuchel akutana na kichapo cha kwanza Bayern Munich

Bayern Munich Lost Tuchel akutana na kichapo cha kwanza Bayern

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bayern Munich imeondolewa kwenye Mashindano ya Kombe la Ujerumani katika hatua ya robo fainali kufuatia kuruhusu bao la jioni walipocheza na Freiburg mchezo uliopigwa Jumanne usiku.

Bayern walianza kufunga bao la kichwa kupitia beki Dayot Upamecano akimalizia mpira wa kiraka Joshua Kimmich kabla ya Nicolas Hoefler kusawazisha dakika nane mbele.

Wakati mchezo ukienda kwenye dakika za lala salama, Bayern Munich inayoongozwa na kocha mpya Thomas Tuchel walisababisha penati ambayo ilitumiwa vizuri na Lucas Hoeler mchezaji wa Freiburg.

Inakuwa mara ya tatu mfululizo kwa Bayern kushindwa kufuzu kucheza nusu fainali ya Kombe hilo wakati Freiburg walifika fainali msimu uliopita wakipoteza kwa RB Leipzig.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live